Tuelimike yatoa elimu kwa wananchi kuelekea uchaguzi serikali za mitaa
25 October 2024, 3:11 pm
Mkurugenzi wa asasi ya Tuelimike kijiji cha isanjandugu halmashauli ya nsimbo Douglas Mwaisaka picha na Lea Kamala
” Wananchi wanapaswa kuchagua kiongozi ambaye atakuwa tayari kushirikiana na jamii yake, mwenye nia na uwezo wa kuwaongoza.”
Na Lea Kamala
Wananchi wa manispaa ya mpanda mkoani Katavi, wameshauriwa kuchagua kiongozi bora ambaye atakuwa tayari kutatua changamoto za wananchi na kuleta maendeleo katika jamii.
Akizungumza na Mpanda Radio Fm kwa njia ya simu, mkurugenzi wa asasi ya tuelimike kijiji cha Isanjandugu kata ya Nsimbo halmashauri ya Nsimbo Douglas Mwaisaka amesema kuwa wananchi wanapaswa kuchagua kiongozi ambaye atakuwa tayari kushirikiana na jamii yake, mwenye nia na uwezo wa kuwaongoza.
Sauti ya Mkurugenzi wa Asasi ya Tuelimike Douglas Mwaisaka
Nao baadhi ya wananchi wa manispaa ya mpanda mkoani Katavi wamesema kuwa kiongozi bora lazima awe mtanzania, awe tayari kuwatumikia wananchi na kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kijamii
Sauti za Wananchi
Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 27 kuchagua mwenyekiti wa serikali za mitaa, kijiji , kitongoji na wajumbe.