Tanganyika wahimizwa kulinda miundombinu inayojengwa
25 October 2024, 2:35 pm
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu, amemtaka mkandarasi kuhakikisha daraja la Ifume linajengwa kwa ubora ili liweze kuwaondolea wananchi wa maeneo hayo kero ya kutumia barabara hususani msimu wa mvua.
Wananchi wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wametakiwa kulinda miundombinu ya barabara inayoendelea kujengwa na serikali katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Moja ya mradi alioutembelea Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu ni ujenzi wa daraja la Ifume linalounganisha vijiji vya Kapalamsenga na Itunya, daraja lenye thamani ya shilingi milioni 700 ambapo amemtaka mkandarasi kuhakikisha daraja hilo linajengwa kwa ubora ili liweze kuwaondolea wananchi wa maeneo hayo kero ya kutumia barabara hususan msimu wa mvua
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TARURA Tanganyika mhandisi Maila Richard Yessaya akizungumza wakati akisoma taarifa ya mradi amesema mradi ulianza 10/05/2024 na unatarajiwa kukamilika 6/11/2024
Kwa upande wao wananchi wa maeneo hayo ambayo ndio walengwa wa miradi hiyo wakizungumza na kituo hiki wamepongeza jitihada za serikali kuendelea kuwaboreshea miundombinu mbalimbali.