Wananchi mtaa wa Mpadeco Katavi walalamikia kutozolewa takataka kwa wakati
15 October 2024, 6:23 pm
“Taka hizo zimekuwa kero kutokana na kukaa bila kuzolewa licha ya kutoa fedha za kutoa takataka hizo katika makazi yao.“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda wamezitaka mamlaka kutatua changamoto ya mrundikano wa uchafu katika makazi.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM ambapo wamesema taka hizo zimekuwa kero kutokana na kukaa bila kuzolewa licha ya kutoa pesa za kutoa takataka hizo katika makazi yao.
Sauti za wananchi mtaa wa Mpadeco wakizungumzia kero ya uchafu katika mtaa wao
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Ivo Chambala amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo inasababishwa na uchache wa magari ya kubeba taka pamoja na ubovu wa miundombinu ya Barabara kuwa ni moja ya sababu zinazosababisha mrundikano mkubwa wa takataka.
Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Ivo Chambala
Hata hivyo jitihada zinaendelea kufanyika ili kuwapata wenye mamlaka husika ambao wanaweza kutolea ufafanuzi dhidi ya changamoto hizo
Sambamba na hilo mwenyekiti Chambala amewataka Wananchi wa mtaa wa Mpadeco kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la wakazi litakalotumika November 27 mwaka huu kuchagua viongozi wa serikali za mitaa.
Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Ivo Chambala