Abiria wanaosafiri na treni Katavi waitaka serikali kuboresha huduma
15 October 2024, 5:54 pm
Stesheni ya Mpanda mkoani Katavi .picha na Rachel ezekia
“Treni mkoani katavi inasafiri mara tatu kwa wiki ikiwa ni pamoja na ukataji wa tiketi katika siku hizo ambazo abiria wanasafiri“
Na Rachel Ezekia -Katavi
Baadhi ya abiria wanaosafiri na treni mkoani katavi wameomba serikali kuboresha huduma zinazotolewa na usafiri huo ikiwemo kuongeza mabehewa ya abria ,huduma ya kielektroniki ya ukataji wa tiketi.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na mpanda redio fm kwa nyakati tofauti wameeleza namna wanavyopata chngamoto ya vitambulisho katika kupata tiketi kutokana na kutokuwa na vitambulisho vya taifa hasa wakitumia barua kutoka kwa wenyeviti wa mitaa.
Sauti ya abiria wakizungumza
Kwa upande wake Emmnueli Mtawali stesheni master mwandamizi stesheni ya Mpanda ameeeleza katika shughuli zote za usafirishaji kuwa treni mkoani katavi inasafiri mara tatu kwa wiki ikiwa ni pamoja na ukataji wa tiketi katika siku hizo ambazo abiria wanasafiri amesema kuwa mikakati ya serikali ni kuhakikisha wanaongeza mabehewa ya abiria pamoja na ukarabati wa njia ya treni.
Sauti ya steshen master Mpanda,Emmanuel Mtawali akizungumza
Stesheni master mwandamizi stesheni ya Mpanda Mtawali picha na Rachel Ezekia
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa abiria kuzingatia taratibu kanuni na sheria za usafiri wa treni kama vile kuwa na vitambulisho ,kufuatilia ratiba za usafiri ,pia changamoto zozote zikitokea ziwasilishwe kwa stesheni master ili zitatuliwe kwa wakati.
Sauti ya stesheni master akitoa wito kwa abiria