Mpanda FM

Wazee Katavi waomba kuimarishiwa huduma za afya

10 October 2024, 4:58 pm

baadhi ya wazee manispaa ya Mpanda

Kuwepo na msisitizo  juu ya matibabu ya bure kwa wazee wasiojiweza kumudu gharama za matibabu.

Na Lazaro Maduhu-Katavi

Baadhi ya wazee wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuhimarishiwa  huduma ya matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM  kwa nyakati  tofauti wakidai kuwepo na msisitizo  juu ya matibabu ya bure kwa wazee wasiojiweza kumudu gharama za matibabu.

Sauti za wazee wakizungumza

Nae Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda Thabiti Malagano amesema serikali imeshatoa msamaha kwa wazee juu ya matibabu huku akitoa utaratibu wake kwa wanufaika hao jinsi ya kupatiwa huduma hiyo bure.

Sauti ya afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda Thabiti Malagano