Katavi waomba maboresho masoko Mpanda hoteli, Matunda
6 October 2024, 11:58 am
Sehemu ya eneo la soko la mpanda hotel
“miundo mbinu hiyo mibovu ya sokoni kama vile ukosefu wa vizimba vya kufanyia biashara na ubovu wa mitaro ya kupitishia maji upelekea kujaa kwa maji sehemu wanazofanyiabiashara hasa wakati wa masika.“
Na Roda Elias -Katavi
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mpanda hoteli na soko la matunda manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa malalamiko yao kuhusiana na miundombinu mibovu ya soko hilo na kutokuwepo kwa usalama wa mazingira katika kipindi cha masika.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wafanyabiashara hao wa soko la Mpanda Hotel na soko la matunda wamesema kuwa miundo mbinu hiyo mibovu ya sokoni kama vile ukosefu wa vizimba vya kufanyia biashara na ubovu wa mitaro ya kupitishia maji upelekea kujaa kwa maji sehemu wanazofanyiabiashara hasa wakati wa masika.
Sauti za wafanyabishara wakizungumza
Kufuatia malalamiko hayo Haji Mponda ambae ni mwenyekiti wa shirikisho la machinga wilaya ya mpanda Akizungumza kwa njia ya simu amewaomba wafanyabiashara kuwa wavumilivu kwasababu serikali inaendelea na ukarabati wa miundo mbinu ya masoko hayo.
Sauti ya mwenyekiti wa shirikisho la machinga wilaya ya Mpanda