Katavi : ACT wazalendo waja na mikakati kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa
24 September 2024, 8:24 pm
picha na mtandao
“Tunatakiwa kujipanga kwa ajili ya kushiriki na kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa “
Na Lilian Vicent -Katavi
Baadhi ya wanachama wa Chama cha ACT wazalendo mkoani katavi wamesema kuwa wamejiandaa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 .
Wameyasema hayo wakati wa mahojiano na Mpanda redio FM katika ofisi za chama hicho zilizopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Sauti za wanachama wa chama cha ACT wazalendo
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho Joseph Mona amesema kwa mujibu wa taarifa za awali wametakiwa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi licha ya kesi iliyofunguliwa na viongozi wao dhidi ya TAMISEMI .
Sauti ya mwenyekiti wa chama hicho Joseph Mona
Ikumbukwe kuwa August 25,2024 Chama hicho kilisema kimejiandaa vyema kushiriki Uchaguzi huo na wameshapeleka kesi Mahakamani kuzuia TAMISEMI ambayo ni Wizara ya Serikali kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.