Wananchi Katavi walilaumu jeshi la polisi, raia kujichukulia sheria mkononi
24 September 2024, 8:03 pm
“Sababu zinazopelekea baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi ni kutokana na baadhi ya watu wanaofanya matukio ya kihalifu kutochukuliwa hatua za kisheria .”
Kutokana na uwepo vitendo vya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuwajeruhi , kuwasababishia vifo kwa baadhi ya watu , wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameliomba jeshi la polisi kuchukua hatua mapema kwa waharifu pindi wanaporipoti matukio ya kiharifu.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM wananchi hao wamesema kuwa sababu zinazopelekea baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi ni kutokana na baadhi ya watu wanaofanya matukio ya kihalifu kutochukuliwa hatua za kisheria .
Sauti za wananchi wakieleza sababu ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi
Kwa upande wake Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi David Mutasya amesema kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kujichukulia sheria mkononi badala yake wanapaswa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa waharifu.
Sauti ya kaimu kamanda wa polisi mkoa wa katavi akizungumza
Hivi karibuni kumeibuka matukio mbalimbali ya wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga na kuwajeruhi baadhi ya watu wakiwatuhumu kuwa ni wezi wa Watoto jambo ambalo ubainika kuwa si sahihi mara baada ya uchunguzi kufanyika hivyo jamii imehaswa kuacha kufanya hivyo.