Mpanda FM

Katavi: Wananchi waja juu takataka kutozolewa kwa wakati

18 September 2024, 11:05 am

Baadhi ya takataka zilizopo kwenye nyumba mbalimbali katika mtaa huo na hazijazolewa.picha na Samwel Mbugi

“wameilalamikia serikali kwa kuto kuzoa taka kwa wakati jambo linaloweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kama vile kipindupindu.”

Na Samwel Mbugi -Katavi

Wananchi wa mtaa wa Kachoma kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamelalamikia kutozolewa taka kwa wakati jambo linaloweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kama vile kipindupindu.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM kuwa taka hizo zimekaa kwa muda mrefu bila kuzolewa jambo ambalo limegeuka kuwa kero kwa wananchi wa mtaa huo.

Sauti ya wananchi wakizungumza

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa kachoma Noel Sokolo amekiri kuwepo kwa taka hizo na kusema kuwa chanzo cha mrundikano huo ni utaratibu mbovu wa kuziondoa kwani wahusika wamekuwa wakichelewa kuzitoa kwa wakati.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa kachoma Noel Sokolo

Hata hivyo Noel amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na mtendaji wa mtaa husika katika kuhakikisha uchafu huo unatolewa kwa wananchi ili kuepusha magonjwa yanayoweza kujitokeza kutokana na uchafu wa mazingira.