Mpanda FM

Kata ya Mpanda Hotel yahamasishwa usafi

2 September 2024, 9:22 pm

picha na mtandao

“kuna baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa hawatoi ushirikiano katika suala la usafi jambo ambalo   halipendezi.

Na Edda Alias-Katavi

Wananchi wa Mtaa wa Mpanda hoteli manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha wanafanya usafi  kwenye  mazingira yanayowazunguka .

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa mtaa huo Christina Mshani  wakati wa kilele cha  kampeni ya usafi iliyoandaliwa na kikundi cha TRANS CARGO.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa huo Christina Mshani akizungumza

Ibrahim Msanda amabaye ni mwenyekiti wa kikundi cha TRANS CARGO amesema usafi umefanyika maeneo mbalimbali lengo likiwa  ni kuhakikisha manispaa inakuwa safi.

Sauti ya Ibrahim Msanda amabaye ni mwenyekiti wa kikundi cha TRANS CARGO

Kwa upande wake  mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda Haidary Sumry  ambaye alikuwa mgeni  rasmi amesema  kuna baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa hawatoi ushirikiano katika suala la usafi jambo ambalo   halipendezi.

Sauti ya mstahiki meya wa manispaa ya mpanda Haidary Sumry

Kilele cha kampeni  hiyo ya  usafi kimefanyika Kata ya Mpanda hotel ambapo kata ya Kashaulili imeongoza kwa usafi huku kata ya  Nsemulwa ikifanya vibaya katika usafi na kupewa kinyago.