Mpanda FM

Katavi: Barua ya mtia nia kugombea nafasi ya ubunge ya pokelewa CHADEMA

2 September 2024, 8:55 pm

picha na mtandao

Hatua hiyo ni kufuatia  tangazo la kuwataka wanachama  kutia nia   ya kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi serikalini  ndani ya  chama .

Na Lilian Vicent -Katavi

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  Sospeter Chotola mkoani Katavi  amepokea barua ya kutia nia ya kugombea nafasi ya ubunge  kutoka kwa mwanachama  Masanja Mussa Katambi .

Akizungumza na vyombo  vya habari  katika ofisi za chama mkoa Chotola amesema hatua hiyo ni kufuatia  tangazo la kuwataka wanachama  kutia nia   ya kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi serikalini  ndani ya  chama .

Sauti ya Katibu wa Chama cha demokrasia na maendeleo  Sospeter Chotola Mkoani Katavi

Masanja mussa Katambi ambaye ametia nia ya kugombea ubunge jimbo la mpanda mjini  amesema amejianda katika Nyanja zote na anaamini akiwa kiongozi atakuwa chachu ya maendeleo.

Sauti ya Masanja mussa Katambi akizungumza

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho jimbo la mpanda mjini amempongeza mwanachama huyo na amewakaribisha wanachama wengine  kujitokeza  kutia ya  kuwani nafasi  jimbo  hilo.

Sauti ya mwenyekiti wa chama hicho jimbo la mpanda mjini