Mpanda FM

Katavi: CCM kata ya Nsemulwa hawajaridhishwa na mkandarasi wa daraja

2 September 2024, 8:25 pm

Wajumbe wa kamati ya siasa wakiwa wametembelea katika daraja ambalo linaendelea na ujenzi

Hawajaridhishwa na mkandarasi wa ujenzi wa daraja la Tulieni kwani hajafuata maagizo ya chama ya kufanya marekebisho.

Liliani Vicent -Katavi

Wajumbe wa kamati ya siasa  Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Nsemulwa  manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema hawajaridhishwa na mkandarasi wa ujenzi wa daraja la tulieni kwani hajafuata maagizo ya chama ya  kufanya marekebisho.

Wameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo ambapo mkandarasi ametakiwa kurudi kujenga kwa kiwango kinachotakiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa kata  hiyo Alex Ngereza amesema  mkandarasi  alipewa maelekezo ya kufanya marekebisho lakini hajafanya hivyo ambapo hatua zitachukuliwa kwa manufaa ya wananchi.

Ziara ya  ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Kata ya nsemulwa   ilianza tarehe 23 mwezi Agost ambapo wametembelea shule ya msingi tulieni na kilimani ,kituo cha afya ,daraja la tulieni na umaliziaji  wa wodi za kinamama.