Wafanyabiashara Katavi wahofia kuuza mahindi NFRA
22 August 2024, 1:04 pm
Picha na mtandao
“Wakulima wengi wana uwezo wa kuzalisha mazao lakini hawana elimu ya kutosha ya kilimo hali inayosababisha wakati mwingine kutokuwa na mazao bora“
Na Lilian Vicent -Katavi
Baadhi ya wafanyabiashara wa mahindi mkoani Katavi wameeleza vigezo vingi vinavyowekwa na NFRA ni moja ya sababu inayopelekea wakulima kushindwa kupeleka kuuza mahindi yao
Wameyasema hayo walipokuwa wakizungumza na mpanda radio FM ambapo wameeleza kuwa wakulima wengi wana uwezo wakuzalisha mazao lakini hawana elimu ya kutosha ya kilimo hali inayosababisha wakati mwingine kutokuwa na mazao bora
Samwel Mlambalike ambaye ni mfawidhi kanda ya Mpanda amesema mahindi wanayonunua ni ya Grade one hivyo wakulima wazingatie ushauri unaotolewa na maafisa ugani ili waweze kupata mazao yaliyo bora.
Ikumbukwe kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Julay 14 2024 alizindua maghala na vihenge vya kisasa vya kuhifadhia nafaka vya Wakala wa Taifa wa hifadhi wa Chakula (NFRA) Mpanda mkoani Katavi ambapo alisisitiza kuwa maghala hayo ni kiashiria tosha kuwa kilimo cha sasa kinahitaji kubadilika na kuwa kilimo cha biashara badala ya mazao ya chakula pekee.