Mpanda FM

Katavi: Maboresho ya barabara wananchi wataka zikamilike kwa wakati

22 August 2024, 9:02 am

picha na mtandao

Wananchi wanatakiwa kutunza miundombinu ya barabara inayoboresha

Na Lilian Vicent-Katavi

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni kuhusiana na maboresho ya barabara yanayoendelea kufanywa na TARURA

Wakizungumza na Mpanda radio FM wamesema kuwa maboresho hayo  ya Barabara yakamilishwe kwa wakati

Sauti ya wananchi wakizungumza kuhusu hali ya barabara .

Kwa upande wake meneja wa TARURA Injinia Kahoza Joseph amebainisha kuwa matengenezo hayo yanafanyika kupitia  fedha za mpango wa matengenezo ya barabara za tozo  za mwaka 2023/2024.

Sauti ya meneja Tarura akizungumza

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu inayoboreshwa kwa kuacha kutupa takataka kwenye mitaro, makaravati  kwani gharama zinazotumika ni kubwa .

Sauti ya meneja Tarura