Katavi: Wafanyabiashara wa samaki watia neno kufunguliwa Ziwa Tanganyika
14 August 2024, 10:59 pm
picha na mtandao
“wanasubiri maelekezo ya waziri mwenye dhamana na sekta hiyo kuhusu ufunguzi wa ziwa Tanganyika na wanachi wataendelea na shughuli zao za uvuvi kama ilivyokuwa hapo awali.”
Na Lilian Vicent- Katavi
Baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wa samaki manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameeleza mapokezi yao kufuatia ufunguzi wa ziwa Tanganyika linalotarajiwa kufunguliwa Agosti 15,2024 .
Wameyasema hayo walipokuwa wanazungumza na Mpanda radio FM na kueleza kuwa wakisubiri kwa muda mrefu ufunguzi wa ziwa hilo kwani hali ya kibiashara imekuwa ngumu kutokana na uchache wa samaki.
Sauti ya wananchi wakizungumza
Nehemia James ni Katibu tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji amesema kuwa wanasubiri maelekezo ya waziri mwenye dhamana na sekta hiyo kuhusu ufunguzi wa ziwa Tanganyika na wanachi wataendelea na shughuli zao za uvuvi kama ilivyokuwa hapo awali.
Sauti ya Nehemia James ni Katibu tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji
Ametoa rai kwa wananchi pindi tu shughuli za uvuvi zitapoanza zitafanyika kwa mujibu wa kanuni ,na taratibu kwaajili kupambana na uvuvi haramu na kuwalinda samaki.
Sauti ya Nehemia James ni Katibu tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji
Ikumbukwe kuwa Serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi ilifunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika tarehe 15 mwezi may mwaka huu kwa lengo la kupumzisha ziwa hilo ili kuwezesha samaki kuzaliana na kuongeza tija kwa wavuvi wanaofanya shughuli zao ziwani humo.