RC Katavi awataka wataalam wa afya kutoa huduma bora
14 August 2024, 10:16 pm
“Serikali kuleta vifaa tiba kunasaidia kuboresha huduma katika sekta ya afya “
Na John Mwasomola- Katavi
Wataalam wa afya wametakiwa kutumia weledi wao na ujuzi walionao katika kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi mkoani Katavi.
Agizo hilo linakuja kufuatia vifaa vya kitaalam ambavyo vinaendelea kutolewa katika hospitali mkoani hapa .
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa vya kupima saratani ya mlango wa shingo ya kizazi .
Aidha amewataka wataalamu hao kuvitunza vifaa hivyo na kuvifanyia matengenezo ya mara kwa mara kulingana na mkataba wake.
Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza
Pia amewataka wanawake kujitokeza Kwenda kufanyiwa utafiti na vipimo ili kujua dalili au tatizo la saratani ya mlango wa shingo ya kizazi, ambapo huduma hizo zinapatikana katika Mkoa wa Katavi tofauti na hapo awali huduma hizo zilikua zinapatikana mikoa ya Jirani.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
Kwa upande wake Kaimu mganga mfawidhi hospital ya rufaa Dkt. Frank Elisha amewashukuru wadau wa afya na serikali, kwa kuwaletea vifaa hivyo ambavyo vinakwenda kuleta sura mpya ndani ya Mkoa na kuahidi kuvitumia kama ilivyokusudiwa.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Rufaa Dkt. Frank Elisha akizungumza
Rose Silvanus ni mwananchi mkoani hapa ameelezea jinsi ilivyokua changamoto hapo awali ya upatikanaji wa huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi .
Sauti ya Rose Silvanus mwananchi mkoani Katavi
Tukio la kukabidhi vifaa vya kupima mlango wa kizazi kwa wanawake limefanyika katika Hospital ya Mkoa wa Katavi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, ambapo zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko.