Mpanda FM

DC Mpanda apiga marufuku kufanyisha kazi watoto katika machimbo

13 August 2024, 9:42 am

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akiwa katika mkutano na wananchi wa kijiji cha dirifu kata ya Magamba . Picha na Anna Milanzi

“Watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kutumikishwa kazi katika migodi, wanafanyiwa vitendo vya ubakaji na ulawiti”

Na Anna Milanzi -katavi

Katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Watoto, wananchi katika Kijiji cha dirifu kata ya magamba wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wamebainisha vitendo vya ukatili  wanavyofanyiwa Watoto katika Kijiji hicho.

Wananchi hao  wameyasema  hayo katika mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda uliofanyika katika kijiji hicho cha Dirifu.

Miongoni mwa mambo ambayo wameyasema ni Pamoja na kuwatumikisha kazi Watoto ambao walipaswa kuwa shuleni

Sauti ya wananchi wa Dirifu wakizungumza juu ya vitendo vya ukatili vinavyoendelea katika maeaneo yao.

Afisa Ustawi wa Jamiia Manispaa ya Mpanda Agness Bulaganya amewataka wazazi na walezi  kuwalinda na kutenga muda wa kuwasikiliza watoto wao ili kujua changamoto zinazowakabili .

Sauti ya Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda Agness Bulaganya

Akizungmza na wananchi hao wa dirifu Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amepiga marufuku vitendo vyote vya ukatili kwa Watoto ikiwemo suala la ndoa za utotoni zinazopelekea mimba za utotoni Pamoja na marufuku ya kuwafanyisha kazi Watoto katika machimbo

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph

Siku za hivi karibuni waandishi wa habari zakupinga vitendo vya ukatili na masuala ya mazingira  mkoani hapa walifika katika kijiji hicho cha dirifu na kubaini uwepo wa vitendo vya ukatili kwa Watoto ikiwemo kufanyishwa kazi katika machimbo yaliyopo katika Kijiji hicho