Mpanda FM

ACT Wazalendo yasikiliza kero za wananchi Katavi

9 August 2024, 10:23 am

mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT wazalendo zuberi zitto kabwe akizungumza na wananchi mkani Katavi.picha na John Mwasomola

Amekutana na kero ya  wananchi kudai kuhamishwa eneo hilo la luhafwe kwa ajili ya  kupisha wawekezaji 26

Na John Mwasomola -Katavi

Kiongozi wa upinzani nchini ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT wazalendo ametembelea kijiji cha Luhafwe  Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi .

Kiongozi huyo amekutana na kero ya  wananchi kudai kuhamishwa eneo hilo la luhafwe kwa ajili ya  kupisha wawekezaji 26 ambao wanataka kulima kilimo cha mbegu  za kisasa za alizeti na mahindi ambapo wao hawatambuliki kama ni wanakijiji au kata lakini wamekuwa wanatozwa fedha na kulipa kodi .

Akiwasilisha hoja hiyo mmoja wa wananchi amebainisha kuwa  wamezunguka ofisi mbalimbali za viongozi wa chama cha CCM mpaka mkoa na kwa viongozi wa serikali bila kupata msaada hivyo wanaona chama cha  ACT wazalendo kitawapa  msaada .

Sauti ya mmoja ya wananchi wa kijiji cha luhafwe

Akijibu kero hiyo Zitto Kabwe amesema wananchi wasiwe na shaka kuhusu hilo ameahidi kwenda kulifanyia kazi na hakuna mwananchi atakayehama eneo hilo.

Sauti ya mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe

Ikumbukwe kuwa katika ziara hiyo wananchi wa kaya mianane wameamua kurudisha kadi za chama cha mapinduzi ccm na kuhamia ACT Wazalendo