SHIDEFA yafanya mdahalo kata ya Intenka kutoa elimu dhidi ya maambuzi ya VVU
16 July 2024, 5:23 pm
“Wataalam wa afya pamoja na shirika la Shidefa Mpanda wameleeza kuwa wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kama matumizi ya dawa ya kinga PEP na kujiepusha ngono zembe“
Na John Benjamin-Katavi
SHIDEFA yafanya mdahalo Kata ya Intenka mkoani Katavi kutoa elimu ya maambukizi dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Baadhi ya wazazi na walezi kata ya Itenka halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni mseto kwa namna gani wanawasaidia watoto kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Wakizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Shidefa Mpanda wameeleza kuwa wamekuwa wakiwapatia elimu ya kujikinga na kujiepusha na mazingira hatarishi ambayo yanaweza kusababisha kuambukizwa virusi hivyo huku wakipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuwapatia elimu ya virusi vya ukimwi.
Aidha baadhi ya vijana wa kata hiyo waliopata nafasi ya kushiriki mdahalo huo wamesema kuwa kupitia elimu ambazo wamekuwa wakipatiwa na watalamu wa afya pamoja na shirika la Shidefa Mpanda ambapo wameleeza kuwa wamekuwa wakitumia njia mbali mbali kama matumizi ya dawa ya kinga PrEP na Kujiepusha ngono zembe
Cleophas Julias msimamizi wa huduma za kinga ngazi ya jamii kutoka shirika lisilo la kiserikali Shidefa Mpanda ameeleza kuwa shirika hilo limekuwa likitoa elimu ngazi ya jamii jinsi ya kujikinga na virusi vya ukimwi kwa kumfikia wananchi moja moja kuptia watoa huduma ngazi ya jamii na kwa kufanya mdahalo mbali mbali kwa makundi tofauti tofauti
Kwa upande wake kaimu mratibu wa ukimwi halmashauri ya Nsimbo wilaya Mpanda mkoani Katavi Baraka Kilima amesema kuwa serikali inaendelea kutoa elimu ngazi ya jamii kupitia zahati,vituo vya afya na shirika la Shidefa Mpanda ambapo amewaomba wananchi kufika katika hayo maeneo kwa ajili ya kupatiwa elimu hiyo.
Shirika la Shidefa Mpanda ni shirika lisilo la kiserikali ambapo limekuwa likitoa huduma na elimu ngazi ya jamii katika masuala kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi na unyanyasaji wa kijinsia.