Mpanda FM

Jeshi la polisi Katavi lapiga msasa madereva wa serikali

16 July 2024, 3:56 pm

Madereva wa serikali wakiwa wanapatiwa mafunzo katika ukumbi wa ofisi za mkurugenzi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.picha na Samwel Mbugi

Kila mtu ana haki ya kutumia barabara, ameongeza kuwa kuna makundi mengi yanapaswa kutumia njia wakiwepo watembea kwa miguu.

Na Samwel Mbugi -Katavi

Jeshi la polis kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Katavi limetoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wanaoendesha vyombo vya serikali ambapo elimu hiyo imetolewa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Katavi RTO Leopard Fungu katika ukumbi uliopo ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda.

Amesema kuwa madereva wanapaswa kuwa makini na kufuata sheria zote za usalama barabaranai kwani kila mtu ana haki ya kutumia barabara ,ameongeza kuwa kuna makundi mengi yanapaswa kutumia njia wakiwepo watembea kwa miguu.

RTO amesema kuwa dereva unapofanya uzembe unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwepo kifo na kupata ulemavu kutokana na dereva kutofuata sheria za usalama na alama za barabarani.

mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Katavi RTO Leopard Fungu akizungumza

Kwa upande wake mkagunzi msaidizi wa polisi kutoka ofisi ya mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Katavi Geofrey Brighton ametaja baadhi ya makosa yanayoweza kusababisha dereva kufungiwa leseni yake ni pamoja na kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha kifo  .

Sauti ya mkaguzi msaidizi wa polisi kutoka ofisi ya mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Katavi Geofrey Brighton akizungumza

Baada ya mafunzo hayo mwenyekiti wa chama cha madereva wa magari ya serikali mkoa wa Katavi Revocatus Mkonje ametoa shukurani kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuwapa elimu ambayo itawasaidia kuepukana na ajari zisizo na ulazima.

Sauti ya mwenyekiti wa chama cha madereva wa magari ya serikali mkoa wa Katavi Revocatus Mkonje akizungumza

Pia mwenyekiti ametoa wito kwa jeshi la polisi kutoa semina kwa viongozi wa serikali, kwani kuna wakati madereva hawapati muda wa kupumuzika jambo linapelekea uchovu unaosababisha ajali nyingi za viongozi wa serikali.