Mpanda FM

Kinana aipongeza jumuiya ya wazazi

12 July 2024, 8:42 am

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana

wazazi ndio msingi wa Malezi na Maadili katika jamiii, hivyo chama cha mapindunzi CCM kinapaswa kusimamia ipaswavyo maadili ya vijana katika makuzi yao.

Na Samwel mbugi -Katavi

Katika mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya wazazi kwa mwaka 2024, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ameipongeza jumuia ya wazazi kwa kuandaa kongamano la maadili na malezi.

Hayo ameyasema katika kongamano hilo lililofanyika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi kuwa muda wote ambao amekitumikia chama hajawahi kuona kongamano kubwa kama lililoandaliwa mkoa wa Katavi.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahiman Kinana

Kinana amesema kuwa wazazi ndio msingi wa Malezi na Maadili katika jamiii, hivyo chama cha mapindunzi CCM kinapaswa kusimamia ipasavyo maadili ya vijana katika makuzi yao.

Sauti ya Makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM )

Hata hivyo mjumbe wa baraza la wazazi taifa viti vitatu bara, Ally Mandai amesema kuwa mmomonyoko mkubwa wa maadili umesababishwa na baadhi ya wazazi kusahau majukumu yao katika kuwalea vijana

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la mpanda mjini Sebastani Kapufi akizungumza na vyombo vya Habari amesema kuwa kongamano hilo limekuwa baraka kubwa sana kwa wanachi wa mkoa wa Katavi ambapo amesema kuna fursa nyingi ambazo wananchi wamezipata kupitia kongamani hilo.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la mpanda mjini Sebastani Kapufi akizungumza

Pia mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi Taska Mbogo ametoa shukurani kwa Rais Wa Jamhuri Ya Mungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kulizia kongamano hilo kufanyika mkoa wa Katavi na imekuwa heshima kubwa sana kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika kufunga Maazimisho ya wiki ya wazani.

Sauti ya mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi Taska Mbogo

Maadhimisho ya jumuia ya wiki ya wazazi kiataifa yalianza tarehe 8 na kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 13 ambapo mgeni rasmi atakuwa ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan