Mpanda FM

Dk Biteko: Umeme wa gridi ya taifa Tabora-Katavi ukamilike Oktoba mwaka huu

11 July 2024, 5:27 pm

picha na Mtandao

kukamilika kwa mradi huo kutaongeza thamani ya uchakataji wa mazao viwandani.

Na Betord Chove

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko, amewataka wasimamizi wa mradi wa umeme wa gridi yaTaifa mkoani Katavi kuacha visingizio na kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo Oktoba mwaka huu.

Dkt. Biteko ameyasema  baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa njia kuu ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Katavi na kituo cha kupokea na kusambaza umeme kilichopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambapo kituo hicho kwasasa kimefikia asilimia 63.

 Sauti ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko

Naye Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza thamani ya uchakataji wa mazao viwandani.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko

Katavi  unatumia umeme unaozalishwa kwa mafuta na mashine za jenereta ambao haukidhi mahitaji ya wananchi na kupelekea changamoto ya kukatika mara kwa mara.