Mpanda FM

Wakuu wa idara Tanganyika watakiwa kujibu hoja zinazoibuliwa na CAG

2 July 2024, 11:13 am

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Charles E. Kichere

Wakuu wa idara na vitengo wenye tabia ya kutoshiriki kujibu hoja zinazoibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni kitendo ambacho kinaibua maswali

Betord Chove -Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kuwasimamia wakuu wa idara na vitengo wenye tabia ya kutoshiriki kujibu hoja zinazoibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kitendo ambacho kinaibua maswali.

Mrindoko ametoa maagizo hayo Juni 29, 2024 kupitia Katibu Tawala wa mkoa wa Katavi Albert Msovela aliyemwakilisha katika mkutano wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Tanganyika wa kupitia na kujadili hoja za Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Sauti ya Katibu Tawala wa mkoa wa Katavi Albert Msovela kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tanganyika  Shaban Juma ameahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizoibuliwa kwa kuunda timu ya utekelezaji.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tanganyika  Shaban Juma

Ikumbukwe ushauri huo umetolewa na CAG. Chambi Sasamka ili kuongeza uwajibikaji katika halmashauri hiyo licha ya kupata hati inayoridhisha.