Mpanda FM

BAKWATA Katavi watoa neno kuhusu uongozi wa Rais Dkt. Samia

2 July 2024, 9:29 am

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan

Amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kupitia Rais Samia Suluhu katika utekelezaji wa maendeleo ya taifa

Na Fatuma Said -Katavi

Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoani Katavi limefanya kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na maendeleo anayoyafanya katika mkoa wa Katavi.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Kakulukulu akizungumza katika swala hiyo maalum amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kupitia Rais Samia Suluhu katika utekelezaji wa maendeleo ya taifa.

Sauti ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Kakulukulu

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Albert Msomera akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, amesema kuwa serikali imepokea fedha kwa ajili ya maendeleo ya mkoa wa Katavi ikiwa ni pamoja  na upande wa  maji, shule na barabara.

Sauti ya Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Albert Msomera