Mpanda FM

Wasafirishaji, wafanyabiashara stand ya zamani Mpanda walia miundombinu ya maji, choo

1 July 2024, 10:33 am

Tank za maji zikiwa katika eneo hilo na hazitumiki wakidai kuwa zimeharibika.Picha na Rachel Ezekea

“Kukosekana kwa miundombinu ya maji na choo kunaathiri utendaji kazi wa wafanyabiashara wa eneo hilo”

Na Rachel Ezekia -Katavi

Baadhi ya madereva wa usafirishaji abiria wa stand ya zamani pamoja na wafanyabiashara waliopo katika eneo hilo manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuboresha miundombinu ya eneo hilo ikiwemo choo na maji.

Wameyasema hayo katika mahojiano na Mpanda Redio fm wamebainisha kuwa miundombinu ya stendi hiyo inaharibu baadhi ya magari  licha ya kuwa wanatoa ushuru bado serikali haifanyi ukarabati kwa wakati

Sauti ya wafanyabiashara na madereva wa stand ya zamani wakizungumza

Kwa upande wake Jofrey Sigulu mwenyekiti wa eneo hilo amebainisha  kuwa amekuwa akifanya jitihada mbalimbali za kufikisha taarifa kwa mkurugenzi kuhusu miundominu ya stendi hiyo pamoja na ukarabati wa choo ambao unaathiri utendaji kazi wa wafanyabiashara wa eneo hilo lakini amekuwa anapewa muda.

Sauti ya mwenyekiti Jofrey Sigulu akizungumza

Nae Festo Tayari katibu wa stendi ya zamani ameiomba serikali kupitia ushuru ambao wanatoa utumike kufanya marekebisho katika eneo hilo  huku wakimuomba mkurugenzi kufika katika eneo hilo ili aone hali ya miundombinu  ilivyo mibovu.

Katibu wa stand ya zamani akizungumza kuhusu hali ilivyo

Mpanda Redio fm inaendelea na jitihada ili kuzungumza na mkurugenzi mtendaji manispaa ya Mpanda aweze kutolea majibu ya changamoto hiyo