Mpanda FM

Wazazi Katavi wasisitizwa kuwapeleka hospitali watoto wenye selimundu

21 June 2024, 10:37 pm

baadhi ya vipimo vya kimaabara .picha na mtandao

kutokana na ukosefu wa elimu wananchi wamekuwa na Imani potofu juu ya ugonjwa huo.

Na Samweli Mbugi -Katavi

Wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa  kuwapeleka Watoto wenye selimundu hospitali kwa ajili ya matibabu na ushauri kwani ugonjwa huo sio wakuambukizwa bali   ni wa kurithi .

Hayo yamesemwa na kaimu mganga mfawidhi hospitali ya manispaa ya  Mpanda  Dkt Mundhiri  Bashiru  wakati akizungumza na Mpanda redio fm  ameongeza kuwa kutokana na ukosefu wa elimu wananchi wamekuwa na Imani potofu juu ya ugonjwa huo.

Sauti ya kaimu mganga mfawidhi hospitali ya manispaa ya  Mpanda  Dkt Mundhiri  Bashiru

Katika hatua nyingine amesema waathirika wakubwa ni kuanzia mtoto wa umri wa miezi sita na kuendelea  na moja ya dalili ni maumivu kwenye vidole na maeneo mengine na kuishiwa damu mara kwa mara

Sauti ya kaimu mganga mfawidhi hospitali ya manispaa ya  Mpanda  Dkt Mundhiri  Bashiru

Baadhi ya wananchi wameeleza uelewa wao juu ya ugonjwa wa  selimundu na ni kwa namna gani unahatarisha maisha endapo hautapata tiba ya hospitali

Sauti za wananchi wakizungumza ambapo wameeleza uelewa wao dhidi ya ugonjwa huo

Maadhimisho ya mwaka huu yamekwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Vunja mduara ,pima, jua hali yako ya sikoseli.