Mpanda FM

Viti mwendo 13 vyakabidhiwa kwa wanafunzi wenye ulemavu manispaa ya Mpanda

16 June 2024, 9:20 am

viti mwendo vilivyotolewa na injinia Ismaili kwa wanafunzi wa shule za msingi wenye ulemavu manispaa ya Mpanda.picha na Ben Gadau

Wananchi ambao wana uwezo wa kuwasaidia watu wenye ulemavu wajitoe ili kuwasaidia na waweze kufikia malengo yao

Na Ben Gadau -Katavi

Mdau wa maendeleo injinia Ismaili ametoa msaada wa viti mwendo 13 kwa watoto wenye ulemavu kwa shule za msingi manispaa ya mpanda mkoani Katavi

Akizungumza wakati wa kukabidhi viti hivyo Eng Ismaili amesema kuwa ameguswa na changamoto ambayo watoto hao wamekuwa wakiupata wakati wanaenda shule kupata elimu.

Sauti ya mdau wa maendeleo injinia Ismaili akizungumza

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Prasido Kameme ameshukuru baada ya kupokea viti hivyo huku akiendelea kuwaasa watu wengine kuiga mfano huo.

Sauti ya mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Prasido Kameme

Wazazi na walezi wa watoto hao wameshukuru huku wakisema viti hivyo vitawarahisishia watoto hao kufika shuleni kwa urahisi kupata elimu.

Sauti ya wazazi wakitoa shukrani mara baada ya kupatiwa viti mwendo kwa ajili ya watoto wao

Viti hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 6 na laki 7 vimetolewa kwa watoto wa shule za msingi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ambapo vitawasaidia katika kupata elimu.