Mpanda FM

Matumizi ya nishati safi ya kupikia kumkomboa mwanamke mkoani Katavi

13 June 2024, 5:53 pm

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.Picha na Fatuma Saidi

Mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia umelenga kumkomboa mwanamke dhidi ya athari zilizopo katika matumizi ya nishati chafu

Na Fatuma Saidi -Katavi

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa katika kuunga mkono jitihada za Serikali kuhusu  mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kutakuwa na kongamano la mwanamke na nishati safi litakalo fanyika tarehe 13.6.2024.

 Mrindoko ameyasema hayo ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari na ameongeza kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi .

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi akizungumzia juu ya mpango huo wa matumizi ya nishati safi ya kupikia

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameeleza uelewa wao juu ya matumizi ya nishati safi huku wakianinisha changamoto ya  gharama  ndio zinazofanya washindwe kutumia na  wameiomba serikali ipunguze gharama za nishati hizo.

Sauti ya wananchi wakieleza namna wanavyotambua umuhimu wa matumizi ya nishati safi na kuomba kupunguzwa bei

Mkoa wa katavi ni mmoja wa mikoa ambayo imekuwa ikitunza mazingira pamoja na misitu  na kupata tuzo mbili katika kilele cha sherehe za mazingira katika halmashauri ya Tanganyika na  kupata hundi ya gawio la vijiji nane katika biashara ya kaboni ambayo ni zaidi Bilioni 14.