Mpanda FM

Ubanguaji karanga wasababisha mafua makali kwa wakazi wa Mpanda

10 June 2024, 2:09 pm

Moja ya takataka zilizotokana na shughuli ya ubanguaji karanga maeneo ya Mpanda Hotel .Picha na Samwel Mbugi

“Wananchi wamelalamikia adha wanayoipata kutokana na kutozolewa kwa taka hizo zilizotokana na ubanguaji karanga katika maeneo hayo ambayo pia yana muingiliano na shughuli zingine za wananchi”

Na Samwel Mbugi Katavi

Baadhi ya wananchi wa kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia adha wanayoipata kutokana na viwanda vya kubangulia karanga vilivyowekwa katika makazi yao.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM kuwa kumekuwa na changamoto ya viwanda hivyo kuzalisha taka ambazo zimekuwa kero na kusababisha kupatwa na ugonjwa wa mafua makali yanayotokana na vumbi linalozalishwa na viwanda hivyo.

 Sauti za Wananchi wanalalamikia vumbi linalotokana na shughuli za ukobaoaji karanga

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpanda Hotel Christina Mshani amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwa amefanya jitihada za kila aina katika kuhakikisha changamoto hiyo inayowakumba wananchi wake inamalizika lakini hadi hivi sasa haijatatuliwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda hotel akitolea ufafanuzi

Hata hivyo mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM amesema kuwa walipokea malalamiko ya wananchi kupitia kwa mwenyekiti wa mtaa na jitihada za vikao vya kuziondoa takataka hizo zilifanyika lakini mpaka sasa hazijazolewa.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM

Aidha mwenyekiti wa CCM amesema kuwa suala hilo kama litaendelea kufumbiwa macho atafanya jitihada za kulifikisha ngazi za juu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.