Mafundi 15 Katavi wapatiwa elimu ya ushonaji mavazi ya kulinia
3 June 2024, 11:29 am
Wahitimu wa mafunzo ya wiki mbili ya ushonaji wa mavazi ya kulinia asali walioshika vyeti pamoja na wakufunzi wao na katibu tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Mkoani Katavi wanne kutoka kulia na kushoto .picha na Betord Chove
“Ushonaji wa mavazi ya kulinia asali yataongeza uzalishaji wa asali na kuwafanya walinaji waweze kulina asali kwa njia salama“
Na Betord Chove -Katavi
Shirika la Enabel kupitia mradi wa BEVAC unaofadhiliwa na umoja wa ulaya Limetoa mafunzo ya wiki mbili kuhusu ushonaji wa mavazi ya kulinia Asali kwa mafundi 15 kutoka halmashauri za wilaya ya Tanganyika,Mlele na Nsimbo mkoani Katavi.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo hayo Katibu tawala msaidizi anaeshughulikia uchumi na uzalishaji Nehemia James amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia ubunifu walioupata kutengeza mavazi yaliyobora ili kuweza kuongeza soko katika sekta ya ufugaji wa nyuki mkoani Katavi na Taifa kwa ujumla.
Sauti ya Katibu tawala msaidizi anaeshughulikia uchumi na uzalishaji Nehemia James
Kwa upande wa wanufaika wa mafunzo hayo kutoka halmashauri tatu za Mlele, Tanganyika na Nsimbo wakizungumza na Mpanda radio fm wamesema mafunzo hayo yatakwenda kuongeza thamani katika sekta ya nyuki kwa kuzalisha mavazi ambayo yatafanya uzalishaji kuongezeka.
Sauti ya wanufaika wa mafunzo hayo kutoka halmashauri tatu za Mlele, Tanganyika na Nsimbo wakizungumza na Mpanda radio fm
Kwa upande wake mratibu mradi wa Bevac Frosia Vugo Sasu Ameeleza matarajio ya mradi baada ya kutoa mafunzo hayo na kuwataka mafundi hao kuyatumia mafunzo hayo ili kuongeza thamani katika sekta ya ufugaji wa nyuki mkoani hapa kwa kutengeneza mavazi bora yatayosaidia katika ulinaji wa asali.
Sauti ya mratibu mradi wa Bevac Frosia Vugo Sasu Ameeleza matarajio ya mradi baada ya kutoa mafunzo hayo
Mradi wa BEVAC unafadhiliwa na Umoja wa ulaya,shirika la maendeleo la ubelgiji, Na nchini unasimamiwa na wizara ya maliasili na utalii ambao unatekelezwa katika mikoa saba nchini ikiwemo Tabora,Kigoma, shinyanga pamoja na mkoa wa Katavi