Wananchi Misunkumilo walia ukosefu wa kituo cha afya
28 May 2024, 12:38 pm
Wamebainisha kuwa kwa sasa huwalazimu kupata huduma za afya katika zahati ya Shule ya wasichana ya Mpanda ama kusafiri hadi mjini kuja kupata huduma hiyo hali ambayo imekuwa ikiwagarimu muda na pesa kwa ajili ya usafiri.”Picha na mtandao
Na John Benjamin-katavi.
Wananchi wa kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda wameiomba serikali kuwajengea kituo cha afya kitakacho wasaidia kupata huduma za afya.
Wananchi hao wakizungumza na Mpanda Redio FM wamebainisha kuwa kwa sasa huwalazimu kupata huduma za afya katika zahati ya Shule ya wasichana ya Mpanda ama kusafiri hadi mjini kuja kupata huduma hiyo hali ambayo imekuwa ikiwagarimu muda na pesa kwa ajili ya usafiri.
Sauti za wananchi wa kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda
Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Mpanda amesema tayari wameshapeleka ombi kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda kwaajili ya kujenga kituo cha afya kata ya Misunkumilo.
Sauti ya Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Kwa upande wa diwani wa Kata ya Misukumilo Matondo Kanyepo amekiri kuwepo kwa changamoto kwa sababu ya ongezeko la watu ndani ya Kata hiyo amekuwa akiwasilisha katika vikao vya bajeti na kuomba kwa mbunge wa jimbo la Mpanda mjini kuweza kusadia upatikanaji wa bajeti kwa ajili wa ujenzi wa kituo cha afya.
Sauti ya diwani wa Kata ya Misukumilo Matondo Kanyepo