RC Mrindoko :Hospitali zinazodaiwa na MSD zilipe madeni
23 May 2024, 10:57 am
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko.Picha na Anna Milanzi
“kulipa madeni katika hospitali ambazo zinadaiwa kutaongeza ufanisi katika utendaji kazi“
Na Rachel Ezekia-Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amezitaka hospitali zinazodaiwa na bohari ya dawa kanda ya magharibi kulipa madeni yote ili kurahisisha utendaji kazi wa bohari ya dawa (MSD) kutoa huduma zao kwa ufanisi .
Mrindoko ameyasema hayo katika kikao kazi cha wadau wa bohari ya dawa kanda ya magharibi mkoa wa Katavi siku za hivi karibuni ambapo lengo kuu ilikuwa ni kuhamasisha utendaji kazi bora .
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
Aidha amewataka bohari ya dawa (MSD) kutoa huduma za dawa katika vituo husika pindi ambapo madeni pamoja na ununuzi wa vifaa kuhakikisha wanazingatia muda ili kutekeleza kazi na maono ya serikali .
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
Kwa upande wake Saraphine Patrice mganga mfawidhi hospitali ya rufaa Katavi amesema wataalamu wa maabara wanafanya kazi kulingana na vitendea kazi pamoja na uwepo wa kutosha wa wataalamu wa dawa na taasisi kutoa ajira za mkataba kulingana na miongozo ya serikali kwa wataalum wa dawa.
Sauti ya mganga mfawidhi Saraphine Patrice