Katavi: Red eyes haina tiba ya moja kwa moja, chukueni tahadhari
3 May 2024, 3:15 pm
Ugonjwa wa macho mekundu mpaka sasa hauna tiba ya moja kwa moja na huchukua siku mbili hadi tano kuona dalili za ugonjwa huu. “Picha na mtandao“
Na Rachel Ezekia-katavi
Wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa macho mekundu [RED EYES] Kutokana na kuathiri watu.
Hayo yamesemwa na daktari wa macho kutoka hospitali ya manispaa ya Mpanda Eckhard Enock ambapo katika katika ziara ya kutoa elimu maeneo mbalimbali wamebaini wagonjwa na kwa siku huwa wanapokea wagonjwa wa macho mekundu watatu hadi wanne kutokana na idadi ya wagonjwa.
Sauti ya daktari wa macho kutoka hospitali ya manispaa ya Mpanda Eckhard Enock akielezea takwimu za wagonjwa wa red eye kwa mkoa wa katavi.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wametoa maoni yao na kuonesha kutokuwa na uelewa wa uhakika kuhusiana na ugonjwa wa macho mekundu.
Sauti za wananchi wakieleza uelewa wao juu ya ugonjwa wa Red eyes
Kwa mujibu wa Enock Ugonjwa wa macho mekundu mpaka sasa hauna tiba ya moja kwa moja na huchukua siku mbili hadi tano kuona dalili za ugonjwa huu.