CHADEMA: maandamano ya amani kufanyika april 24 mkoani Katavi
21 April 2024, 1:17 pm
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA .Picha na Lilian vicent
“chama cha demokrasia na maendeleo kimejipanga kwa kuandaa mwanasheria atakaesimamia kesi za migogoro mbalimbali ambayo wananchi wa mkoa wa Katavi wanaonewa bila kupewa haki yao.“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Katavi kimeendelea na hamasa ya maandamano ya amani yatakayofanyika Manispaa ya Mpanda aprili 24,2024 kwa lengo la kudai katiba mpya na ugumu wa maisha kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa chama cha CHADEMA mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela akiwa wilaya ya Tanganyika kata ya Kasekese kuwa miongoni mwa mambo ambayo yanayosababisha kuandamana ni migogoro inayofanywa na watu wachache wakiongozwa na chama cha mapinduzi CCM.
Sauti ya mwenyekiti wa chama cha CHADEMA mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela
Pia amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuandamana kutokana na sababu ya Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania pamoja na wateule wake akiwemo Mbunge wa jimbo la Tanganyika kushindwa kutetea masilahi ya wananchi.
Sauti ya Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA mkoa wa Katavi akieleza sababu za kufanya maandamano
Rhoda ameongeza kuwa chama cha Demokrasia na maendeleo kimejipanga kwa kuandaa mwanasheria atakaesimamia kesi za migogoro mbalimbali ambayo wananchi wa mkoa wa Katavi wanaonewa bila kupewa haki yao.
Sauti ya mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa katavi akizungumza
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Katavi Oscar George Sangu amesema kuwa kipindi hiki chama cha mapinduzi CCM kimeanza kuwatumia watumishi wa serikali kuwa viongozi wa chama wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari ambapo ni kinyume na maadili ya kazi.
Sauti katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Katavi Oscar George Sangu
Nae katibu wa wilaya ya Tanganyika Thomas Masanja amesema kuwa serikali ya chama cha mapinduzi imesababisha migogoro kutokana na watendaji wa serikali kuachiwa majukumu ambayo yanapaswa kufanywa na ngazi zingine lakini wao wamekuwa wakifanya kinyume cha sheria .
Sauti ya katibu wa wilaya ya Tanganyika Thomas Masanja akizungumza
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo amesema kuwa mkoa wa Katavi umejipanga kufanya maandamano yatakayofanyika mkoani hapa kuanzia tarehe 24 mwezi huu ambapo kwa mkoa wa Katavi yatafanyika Manispaa ya Mpanda.