Rais wa chemba ya wafanyabiashara nchini azitaka taasisi binafsi kuungana
19 April 2024, 11:41 pm
Rais wa chemba ya wafanyabiashara Tanzania [TCCIA] Vicent Bruno Minja akizungumza na wafanyabiashara mkoani Katavi.Picha na Veronika Mabwile
“changamoto zinashindwa kutatuliwa kutokana na wafanyabiashara wenyewe kutokuwa na umoja“
Na Veronika Mabwile -Katavi
Rais wa chemba ya wafanyabiashara Tanzania [TCCIA] Vicent Bruno Minja amezishauri Taasisi binafsi Mkoani Katavi kuungana ili kusaidia kuongeza uzito kwa serikali katika kutatua changamoto zinazo zikabili taasisi hizo .
Ushauri huo ameutoa wakati wa kikao na wafanyabiashara kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda na kusema kuwa changamoto zinashindwa kutatuliwa kutokana na wafanyabiashara wenyewe kutokuwa na umoja
Sauti ya Rais wa chemba ya wafanyabiashara Tanzania [TCCIA] Vicent Bruno Minja
Kwa upande wao wafanyanyabiashara waliohudhuria kikao hicho wamezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo miundombinu mibovu ya barabara ambayo wamesema inachangia ucheleweshwaji wa mizigo
Sauti ya wafanyanyabiashara waliohudhuria kikao hicho wakitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili
Viongozi wa Chemba ya biashara Mkoani hapa wamesema kuwa wanamkakati wa kuanzisha dawati la kikodi kwa lengo la kuwasaidia wafanyabiashara kutatua changamoto zitokanazo na malipo ya kodi.
Sauti ya Viongozi wa Chemba ya biashara Mkoani Katavi
Rais wa chemba ya wafanyabiashara hapa nchini anafanya ziara ya kutembelea mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa lengo la kusikiliza kero na kutazama fursa zilizopo katika mikoa hiyo.