Mwenyekiti Chadema mkoa wa Katavi atangaza maandamano
19 April 2024, 12:03 pm
Mwenyekiti wa Chama cha Chadema mkoa wa Katavi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Picha na Lilian Vicent
“tuna mambo makuu manne ikiwamo jambo la maandamano ambapo wiki ya maandamano inaanza tarehe 22 mwezi wa nne na jambo hili la maandamano lina umuhimu mkubwa,serikali inatakiwa irekebishe mambo mbalimbali”
Na Lilian Vicent-Katavi
Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema wanatarajia Kuanza wiki ya maandamano kuanzia april 22 mwaka 2024
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa katavi Rhoda Kunchela ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari ,viongozi pamoja na wajumbe wa chama hicho uliofanyika katika ofisi za Chadema mkoani hapa na kuongeza kuwa unyonywaji unaofanywa kwa wachimbaji wadogo ni sababu inayochangia maandamano.
Sauti ya Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa katavi Rhoda Kunchela
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali wamesema wanaunga mkono na watahamasisha wananchi kujitokeza kuandamana .
Sauti ya viongozi wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali
Nao wanachama walihodhuria kikao hicho wamesema kuwa wao wamepokea kauli ya viongozi wao na wanahitaji tume huru itakayosimamia uchaguzi kwa haki.
Sauti ya wanachama waliohudhuria kikao hicho
video ya habari hii inapatikana katika youtube channel yetu bofya hapa kutazama.