Katavi, Kiasi cha Tshs Milioni Sita chatolewa Katika Mtaa wa Kilimani Kwa ajili ya Ujenzi wa Shule
8 April 2024, 1:39 pm
Picha na Mtandao
“Baada ya kuzipokea Fedha hizo alikaa na Wajumbe kwa ajili ya kufanya Maamuzi, wakaona ni Vyema kuwashilikisha Wananchi ili kukubaliana kiasi cha kuchangia kwa ajili ya upatikanaji wa Mchanga“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Wananchi wa Mtaa wa Kilimani Kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamepokea Fedha Kiasi cha Tshs Million Sita kutoka ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi inayotarajiwa kuanza kujengwa hivi Karibuni.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji wa Kata ya Nsemulwa Ruben Kasomo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Kilimani ambapo amesema wamepokea Barua kutoka kwa Mkurugenzi inayoainisha kupewa kiasi hicho cha Fedha.
Sauti Mtendaji wa Kata ya Nsemulwa Ruben Kasomo akizungumza
Aidha Kasomo amesema kuwa Fedha hizo ni kwa ajili ya Ununuzi wa Vifaa ambavyo vitatumika katika Ujenzi huo ikiwemo Saruji na Misumari.
Sauti ya Mtendaji wa Kata ya Nsemulwa Ruben Kasomo
Nae Mwenyekiti wa Mtaa huo Florence Mbangule amesema kuwa baada ya kuzipokea Fedha hizo alikaa na Wajumbe kwa ajili ya kufanya Maamuzi, wakaona ni Vyema kuwashilikisha Wananchi ili kukubaliana kiasi cha kuchangia kwa ajili ya upatikanaji wa Mchanga.
Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa huo Florence Mbangule akizungumza
Hata hivyo Serikali ya mtaa huo na Wananchi wamekubaliana Mwisho wa Mchango huo itakuwa ni tarehe 30 ya Mwezi wa tano mwaka huu ili kila Mwanachi awe ametoa kiasi cha shilingi elfu tano.