Wizi koki za maji Katavi chanzo cha kukosekana huduma ya maji
2 April 2024, 10:23 pm
Picha na Mtandao
Wizi wa koki uliokuwa unafanywa na wahalifu ulichangia kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa maji katika mtaa wa Mpanda hoteli.
Na Samwel Mbughi-Katavi
Wananchi wa Mtaa wa Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa Shukrani kwa Serikali baada ya kutatua changamoto ya Maji iliyokuwa inawakabili katika eneo hilo .
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Redio Fm na kuongeza kuwa wizi wa koki uliokuwa unafanywa na wahalifu ulichangia kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa Maji katika mtaa huo.
Picha na Mtandao
Sauti ya wananchi mtaa wa Mpanda hotel
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Christina Mshani amesema wameshirikiana kwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na chama kuhakikisha huduma ya Maji inarejeshwa kwa wakati.
Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpanda hoteli
Nae Diwani wa kata ya Mpanda hoteli Hamisi Richard Misigalo amebainisha kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada kuhakikisha maeneo ambayo maji hayajafika yanafika kwa wakati .
Sauti ya Diwani Kata ya Mpanda hoteli
Hata hivyo Misigalo ameishukuru Mpanda Radio Fm kwa kuendelea kufuatalia maendeleo ya kata ya Mpanda hoteli, ambapo amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Wananchi ambao huduma ya Maji haijawafikia inawafikia.