Wanawake Katavi wapanda miti kutunza mazingira
7 March 2024, 3:29 pm
“Miti hiyo inayopandwa itakuwa ni kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya mwanamke mwaka huu lakini pia ni sehemu uendelezaji wa utunzaji mazingira mkoani hapa“
Na Deus Daud-katavi
Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani manispaa ya Mpanda imefanya zoezi la upandaji miti katika shule ya sekondari Mtemibeda kwa lengo la kuendelea kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa jamii.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Mpanda bi Malieta Mlozi amesema kuwa miti hiyo inayopandwa itakuwa ni kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya mwanamke mwaka huu lakini pia ni sehemu ya uendelezaji wa utunzaji mazingira mkoani hapa.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) FORTINATUS KABEJA mkoa wa katavi amesema kuwa ni muhimu kwa watu kuendelea kuwa na nidhamu ya maisha ili kuweza kufanikiwa katika maisha yao.
“Sauti ya Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) FORTINATUS KABEJA mkoa wa katavi akiwaasa wanawake kuwa na nidhamu ya maisha ili kufanikiwa”
Siku ya Mwanamke Duniani huazimishwa ifikapo tarehe 8.mwezi wa tatu kila mwaka na mwaka huu imebebwa na kauli Mbiu isemayo “wekeza kwa wanawake hakikisha maendeleo ya taifa na usitawi wa jamii”
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo wakipanda miti . Picha na Deus Daud