Maoni ya Wananchi juu ya Katazo kwa Madalali
20 November 2021, 1:06 pm
Baadhi ya wananchi manispaa ya mpanda mkoani katavi wamekuwa na maoni tofauti juu ya katazo la madalali wa nyumba kupewa kodi ya mwezi mmoja.
wakizungumza na mpanda radio fm wananchi hao wameleza kufurahishwa kwa marufuku hiyo huku wengine wakionesha kutoridhishwa na maamuzi hayo.
kwa upande wake israeli mwaipopo ambae ni dalali wa nyumba ameeleza moja ya changamoto wanayokutana nayo ni wamiliki wa nyumba kutokukubali kulipa asilimia kumi ya kodi wanayopangisha hali inayowapelekea kuomba pesa hiyo kutoka kwa wapangaji.
Hivi karibuni waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepiga marufuku kwa madalali wa nyumba wanaochukua kodi ya mwezi mmoja kwa wapangaji kuacha tabia hiyo na badala yake pesa hizo zilipwe na wenye nyumba.