Hifadhi ya Katavi na Utajiri wa Viboko
20 November 2021, 12:25 pm
Hifadhi ya taifa mkoani katavi inatajwa kuwa moja ya hifadhi inayoongoza kuwa na viboko wengi afrika huku idadi ya viboko hao ikikadiriwa kuwa ni zaid ya milioni mbili .
Hayo yamebainishwa na muongoza watalii katika hifadhi hiyo God listern Isaya katika ziara ya waandishi wa habari mkoani humo iliyoandaliwa na mbunge wa mpanda mjini sebastian kapufi na kueleza kuwa uwepo wa viboko hao umeifanya hifadhi hiyo izidi kutambulika afrika.
Aidha mbunge wa mpanda mjini Sebastian Kapufi amewasisitiza waandishi wa habari kuendelea kuitangaza hifadhi hiyo huku akiwataja waandishi hao kuwa ni moja ya makundi yanayosikilizwa katika jamii.
baadhi ya waandishi wameomba mamlaka kuendelea kutangaza utalii wandani ili utambulike zaidi na hatimae kukuza uchumi wa mkoa na taifa kiujumla.
Hifadhi ya taifa ya katavi mbali kuwa ni hifadhi yenye viboko wengi afrika bali ni hifadhi pekee duniani anayopatikana twika mweupe.