Jamii FM

DCEA Kanda ya Pwani kutoa elimu kupitia Samia legal aid campaign Mtwara

26 January 2025, 15:23 pm

Julius Beuta Kiza akielezea namna walivyojipanga kutoa elimu ya athari na madhara ya matumzi ya dawa za kulevya katika jamii(Picha na Musa Mtepa)

Dhamira ya Mamlaka ya kuthibiti na kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) kanda ya pwani ni kutoa Elimu kwa Jamii juu ya athari na madhara yake kupitia  Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia inayoendelea kutolewa viwanja vya Mashujaa Manispaa ya Mtwara Mikindani

Na Musa Mtepa

Katika kuhakikisha matumizi bora ya siku kumi za kutoa msaada wa kisheria kupitia kampeni ya msaada ya kisheria ya Mama Samia, Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) Kanda ya Pwani imejizatiti kutumia fursa hii kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara na athari zinazotokana na matumizi ya dawa za kulevya katika jamii.

Akizungumza na Jamii FM Radio wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Pwani, Bw. Julius Beuta Kiza, amesema kuwa mamlaka hiyo imeamua kutumia kipindi hiki cha kampeni ya msaada wa kisheria kutoa elimu kwa umma kuhusu athari na madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Sauti ya 1 Julius Beuta Kiza afisa wa DCEA kanda ya pwani.

Bw. Kiza ameeleza kuwa athari kubwa zinazojitokeza kutokana na matumizi ya dawa za kulevya ni pamoja na kusambaratika kwa familia na kupoteza nguvu kubwa ya taifa, hasa vijana ambao ni nguzo muhimu ya uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.

Sauti ya 2 Julius Beuta Kiza afisa wa DCEA kanda ya pwani.

Pia, ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kuhusu uwepo wa watumiaji, wafadhili, walimaji, na wasambazaji wa dawa za kulevya kwa kutumia namba 119 ili mamlaka iweze kuchukua hatua za haraka na kuokoa jamii kutokana na madhara hayo.

Kwa upande mwingine, Bw. Kiza amesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi katika kutoa taarifa ni muhimu ili kudhibiti wimbi la matumizi ya dawa za kulevya na kuhakikisha jamii inakuwa salama.

Sauti ya 3 Julius Beuta Kiza afisa wa DCEA kanda ya pwani.

Kampeni ya msaada ya kisheria ya Mama Samia inatarajiwa kuendelea kutoa huduma za kisheria na elimu kwa jamii kwa siku kumi mfululizo, huku DCEA ikilenga kupunguza madhara ya dawa za kulevya na kuimarisha ufanisi wa utoaji wa Elimu kwa jamii juu ya athari na madhara yake kwa jamii na taifa kwa ujumla.