Jamii FM

Vijana mkoani Mtwara watakiwa kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi

23 July 2024, 14:22 pm

Judith Chitanda na Fabian Msumanje kutoka Nerio Paralegal Mkoa wa Mtwara wakiwa katika studio za jamii fm redio wakizungumzia juu ya vijana kushirika katika michakato ya uchaguzi(Picha na Musa Mtepa)

Kitendo cha kuchagua kiongozi unayemtaka kinaleta faida kwasababu unampata kiongozi anayeweza kuleta maendeleo katika jamii kwa kusimama na kukusemea malengo ya jamii husika.

Na Musa Mtepa

Vijana mkoani Mtwara wametakiwa kushiriki katika michakato mbalimbali ya uchaguzi na uongozi kwa kuanzia katika hatua za awali ili kumpata kiongozi anayehitajika na jamii na anayeweza kutatua kero zinazowazunguka wananchi.

Wito huo umetolewa na afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Nerio Paralegal kwa niaba ya Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi Judith Chitanda kwenye kipindi cha dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii fm radio ambapo amesema kuwa hivi karibuni kutakuwepo zoezi la uhakiki wa daftari la kudumu la wapiga kura hivyo ni wakati  kwa jamii hususani vijana kuboresha taarifa zao ili kuwa na haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka.

Sauti ya Judith Chitanda Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Nerio Paralegal Mtwara.

Aidha Judith Chitanda na Fabiani Msumanje amesema Pamoja na vijana kuwa katika harakati za kutafuta Maisha hasa maafisa usafirishaji (Bodaboda) wanatakiwa kutenga muda kwa ajili ya kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao ili kuondokana na kitendo cha kujitokeza kwa uwingi katika kumpamba mgombea wakati wa kampeni kuliko kupiga kura.

Sauti ya Bi Judithi Chitanda afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Nerio Paralegal Mtwara na Bw Fabian Msunje kutoka Nerio
Judith Chitanda,Fabian Msumanje na Grace Hamisi wakiwa katika kipindi cha dira ya asubuhi wakijadili juu ya namana vijana wanavyotakiwa kushiriki katika michakato ya uchaguzi kupitia vipindi vya haki mlinzi vilivyopo chini ya LHRC(Picha na Musa Mtepa)

Pamoja na hayo Judith Chitanda amewaasa vijana kuacha tabia ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu zaidi moja ili kuepuka adhabu zinazoweza kujitokeza kutokana na kitendo hicho.

Sauti ya Judithi Chitanda afisa ufuatilaji na tathmini kutoka Nerio Paralegal Mtwara.