Jamii FM

Waziri Stergomena Tax Atekeleza Ahadi ya Kompyuta Mtwara

16 October 2024, 16:17 pm

kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara kwa niaba ya Waziri wa ulinzi akikabidhi Kompyuta kwa mkuu wa wilaya ya Newala Al-hajj Rajab Kundya ikiwa utekelezaji wa ahadi zilizotolewa akiwa ziarani mkoani Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Hivi karibuni Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Stergomena Tax alifanya ziara mkoani Mtwara ya kutembelea,kukagua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi mbalimbali inayotekelezwa  na baadhi yake kuahidi kutoa mchango wake.

Na Musa Mtepa

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, amekabidhi kompyuta 30 kwa shule tatu za sekondari na shilingi milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya Kijiji cha Maparawe wilayani Masasi ikiwa utekelezaji wa ahadi za  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Stergomena Tax, alipofanya ziara mkoani humo.

Shule zilizopokea kompyuta ni pamoja na Shule ya Sekondari Mustafa Sabodo, Shule ya Sekondari Nanda, na Shule ya Sekondari Tulindane.

Sauti ya 1 Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara

 Katika hotuba yake, Kanali Sawala ametoa shukrani kwa Waziri Tax na kuwasihi wakuu wa wilaya na wasaidizi wao kuhakikisha kompyuta hizo zinatunzwa vyema ili ziweze kusaidia vijana kupata maarifa mapya yatakayo wasaidia kufanya vizuri .

Sauti ya 2 Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara
Wakurugenzi,wakuu wa shule na baadhi ya viongozi wakifuatilia hafla ya kukubidhi kumpyuta 30 zilizotolewa na waziri wa ulinzi(Picha na Musa Mtepa)

Wakuu wa shule hizo wamepongeza hatua hiyo na kuahidi kuziweka kompyuta hizo katika hali nzuri, wakiamini kuwa zitaleta ufanisi mkubwa katika masomo ya wanafunzi.

Sauti za Walimu wakuu wa shule za sekondari zilizopewa zawadi ya kompyuta kutoka Waziri Stergomena Tax.