Wakazi wa Mjimwema wakabiliwa na ukosefu wa maji
14 October 2024, 11:13 am
Licha ya kuwa Mjimwema ndipo yalipo matenki ya maji yanayotoka katika chanzo cha maji cha Lwelu wananchi wanashangazwa na kuadimika kwa huduma hiyo.
Na Musa Mtepa
Wakazi wa Mjimwema katika kata ya Magengeni, Manispaa ya Mtwara Mikindani wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa huduma ya maji.
Wanalazimika kutembea zaidi ya kilometa 3 hadi Mawangwa ili kupata huduma ya maji, licha ya juhudi za MTUWASA kuleta huduma hiyo.
Amina Said Mdingila, mmoja wa wakazi wa mtaa wa huo, ameiomba serikali kuwasaidia ili wapate maji ya kutosha ili kuondokana na kadhia wanayoipata hivi sasa.
Mzee Sadiki, msambazaji wa maji kupitia matenki ya eneo hilo, anasema udogo wa tenki lililojengwa kwa ajili ya wakazi wa mtaa huo unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa changamoto hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Filbert Magaga, amethibitisha changamoto hii na tayari ameshawasilisha malalamiko ukosefu wa maji kwa mkurugenzi wa MTUWASA na kuahidi kuendelea kufuatilia hadi wananchi watakapopata huduma ya maji kwa uhakika.