ADEA, UNESCO watangaza mafunzo ya bure kwa vijana Mtwara Mikindani
12 November 2024, 17:34 pm
Mkoa wa Mtwara ni mkoa adhimu katika sanaa ya uchongaji wa vinyago hivyo kama rasilimali hizi zikitumika vizuri na vijana zinaweza kuwakomboa kiuchumi na hivyo kuwaezesha kujitegemea na kujenga taifa imara .
Na Musa Mtepa
Vijana wametakiwa kujitokeza kwa uwingi katika mafunzo ya kuimarisha sanaa,utamaduni na ufundi stadi yaliyoandaliwa na shirika linalojihusisha na sanaa na utamaduni mkoani Mtwara la ADEA kwa kushirikiana na UNESCO ili kujiongezea elimu na ujuzi utakao wasaidia kufanya kazi mbalimbali na kujiongezea kipato katika Maisha yao.
Hayo yamesemwa November 11, 2024 na Mgeni rasmi ,Bi Fatuma Mtanda afisa utamaduni mkoa wa Mtwara kwenye uzinduzi wa program ya kuimarisha sanaa,utamaduni na ufundi stadi kwa vijana yaliyofanyika katika viwanja vya Mkanaledi Manispaa ya Mtwara Mikindani, ambapo Bi Fatuma amewataka vijana kujitokeza kwa uwingi na kushawishika katika mafunzo hayo yatakayotolewa bure kwa vijana 50 ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Aidha Fatuma Mtanda amewaomba viajana watakaoshiriki mafunzo hayo kufanya kazi kwa juhudi na maarifa wakati wa mafunzo na baada ya mafunzo watakapo tumia ujuzi huo ili kuwavutia wateja katika kazi zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ADEA Saidi Chilumba amesema mafunzo hayo maalumu yatatolewa katika fani nne za mikono ambazo ni Uchoraji,uchongaji,ufundi selemala na ufundi chuma ambapo takribani vijana 50 watanufaika na mafunzo hayo.
Saidi Chilumba amesema kuwa sababu kubwa iliyopelekea kuandaa mafunzo hayo kwa vijana ni pamoja na wengi wao kujisahau kuwa kuna Maisha baada ya ujana huku wengi wao wakijikita katika fursa za bodaboda ambazo sio endelea kwa Maisha ya baadae.
Naye Elias Mzunda kaimu mratibu wa mafunzo kwa vyuo vya ufundi stadi (VETA) kanda ya mashariki inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kupata mafunzo hayo na wao kama VETA watashirikiana kikamilifu na ADEA katika kuhakikisha kile ambacho wanapasa kukipata kinapatikana.
Nao baadhi ya vijana na wazazi waliofika katika utambulisho huo wameonesha kufurahishwa na fursa hiyo na kuwaomba vijana kujitokeza kwa uwingi katika mafunzo .