Jamii FM

Wazazi, walezi Mtwara wasisitizwa kutimiza haki na mahitaji ya watoto

5 December 2024, 12:06 pm

Selemani Mkuchika na Fabian Mumanje kutoka Nerio Paralegal kwa niaba ya LHRC wakitoa Elimu juu ya matunzo ya watoto(Picha na Mwanahamisi Chikambu)

Hii ni katika kutimiza majukumu ya wazazi na walezi kwa watoto ikiwa katika kutimiza majukumu na haki za watoto katika nyanja mbalimbali za malezi.

Wazazi na walezi mkoani Mtwara wametakiwa kufahamu haki za watoto na kutimiza mahitaji ya mtoto ili awe na afya njema, apate elimu, na ashiriki katika ujenzi wa taifa lake atakapokuwa mtu mzima.

Hayo yameelezwa na Afisa Uhamasishaji na Tathmini kutoka Nerio Paralegal kwa niaba ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Selemani Mkuchika, katika kipindi cha Dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii FM Radio. Mkuchika amesema kuwa mtoto asipotimiziwa mahitaji yake ya msingi, mzazi anapaswa kushitakiwa.

Sauti ya 1 Selemani Mkuchika afisa uhamasishaji na Tathmini kutoka Nerio Paralegal

Aidha, Mkuchika ameongeza kuwa mtoto ana wajibu wa kusaidia kazi za nyumbani ili kumjengea uwezo wa kuwajibika na kukuza uwezo wake.

Sauti ya 2 Selemani Mkuchika afisa uhamasishaji na Tathmini kutoka Nerio Paralegal

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji kutoka Nerio Paralegal, Fabian Mumanje, amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwapeleka watoto kwa bibi zao ili waweze kupata haki zao za msingi.

Sauti ya 1 Fabiani Msumanje Mkurugenzi Mtendaji kutoka Nerio Paralegal

Mumanje pia amewataka wazazi na walezi ambao wameachiwa kulea familia peke yao kufika katika vyombo vya sheria na Nerio Paralegal ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

Sauti ya 2 Fabiani Msumanje Mkurugenzi Mtendaji kutoka Nerio Paralegal