Jamii FM

Waziri wa Kilimo azindua ujenzi wa maabara ya TARI Naliendele

2 October 2024, 20:59 pm

Jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa Maabara ya utafiti wa Mazao TARI -Naliendele(Picha na Mwanahamisi Chikambu)

Maabara hayo yatasaidia katika kufanya tafiti mbalimbali katika kituo cha TARI Naliendele ikiwa katika magonjwa na mbegu bora inayoweza kuhimili katika mazingira yote.

Na Mwanahamisi Chikambu

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, amezindua rasmi ujenzi wa maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele, mkoani Mtwara.

Maabara hii itakuwa na jukumu muhimu katika kufanya tafiti zinazohusiana na magonjwa ya mimea.

Waziri Bashe amewataka watafiti wa TARI Naliendele kuendeleza juhudi zao, huku akiwapongeza kwa kutekeleza tafiti na kugundua mbegu bora licha ya changamoto za ukosefu wa mfumo wa fidia kwa kazi zao.

Sauti ya Husein Bashe Waziri wa kilimo

Aidha Waziri Bashe amesisitiza umuhimu wa uzalishaji wa mbegu za asili katika msimu wa mvua unaotarajiwa hivi karibuni , ili wakulima waweze kuchagua mbegu wanazohitaji.

Sauti ya 2 Husein Bashe waziri wa kilimo

Katika taarifa, watafiti wa TARI Naliendele wameonyesha kwamba wamefanikiwa kugundua mbegu mbalimbali za korosho, mbolea bora, na hata njia za kutengeneza mvinyo kutoka kwenye tunda la korosho. Ujenzi wa maabara hiyo utaongeza ufanisi wa tafiti katika kituo hicho na kusaidia vituo vingine vya TARI nchini.

Kituo cha TARI Naliendele kinajulikana kama mojawapo ya vituo 17 vya TARI nchini, kikiwa na hekta 3151.32 za matumizi ya tafiti.

Awali, kituo hiki kilikuwa na ekari 165 zinazozalisha tani 100, lakini sasa kimefanikiwa kuongeza eneo hilo hadi ekari 363, ambapo kinatarajiwa kuzalisha tani 220.

 Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya kilimo nchini Tanzania.