Mafundi chuma Mtwara wapata mafunzo ya kuongeza ubunifu
1 December 2024, 14:13 pm
Hili ni kundi la nne na la mwisho katika program ya kuimairisha sanaa,na utamaduni katika ufundi stadi yanayotolewa na shirika la ADEA
Na Musa Mtepa
Mafunzo ya kuimarisha sanaa na utamaduni kupitia ufundi satadi katika kutengeneza ajira yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la ADEA mkoani Mtwara kwa kufadhiliwa na UNESCO na Alwaleed Philanthropies yameendelea kutolewa November 30,2024 kwa baadhi ya mafundi chuma wanaopatikana Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Wakizungumzia mafunzo hayo baadhi ya mafundi chuma wamesema kuna mambo mengi wanaendelea kujifunza ikiwemo namna ya kumjali mteja,kutengeneza bidhaa iliyo bora pamoja na kuwa ubunifu wa kazi mbalimbali.
Abdulaaziz Ahmadi Fundi Chuma kutoka Mkanaledi Manispaa ya Mtwara Mikindani amesema kupitia mafunzo hayo yatakuwa na faida kubwa kwani atawashirikisha vijana wengine waliopo katika kiwanda chake ili kuwasaidia katika masoko pamoja na utengenezaji wa bidhaa tofauti na za kipekee na mafundi wengine.
Akizungumzia changamoto anazokutanazo katika shughuli zake za uchomeleji Abdulaziz amesema kuwa kuna baadhi ya wateja kuzoea kufanya kazi za bei rahisi bila kuangalia ubora na faida yake katika bidhaa husika.
Godlove Mselewa na Mahibu Ahmadi ni wanafunzi wa ufundi chuma (Uchomeleaji) wanaofanya kazi zao Manispaa ya Mtwara Mikindani wamesema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia katika uboreshaji wa kazi zao wanazo zalisha kila siku huku wakiwasihi vijana kujitokeza kwa uwingi pale zinapotokea fursa za kukuza ujuzi katika kazi zao wanazo zifanya.
Omari Mchelenga Mwezeshaji amesema mapokeo ya Wanafunzi katika mafunzo hayo ni mazuri na matarajio yake ni kuona baada ya mafunzo wanaenda kuzalisha bidhaa iliyobora na yenye utofauti na mafundi wengine ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
kwa upande wake Saidi Chilumba Mkurugenzi wa ADEA amesema mafunzo hayo yanayohusisha makundi ya uchoraji,uchongaji,useremala na ufundi chuma yanazingatia zaidi katika suala la ubunifu na kukuza sanaa katika bidhaa zinazo zalishwa.
Aidha amesema mafunzo hayo ni ya miezi sita ambapo kwa awamu ya kwanza yatachukua miezi miwili na tayari wameanza kutoa mafunzo hayo katika fani zote nne huku mwitikio ukiwa mkubwa na kupongeza zaidi katika mafunzo hayo uwepo wa Wanawake wanaoshiriki.