Jamii FM

Nyumba yateketea kwa moto Mtwara

1 November 2024, 09:09 am

Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mtwara ,Mrakibu Msaidizi Oissa Silingi akitoa taarifa juu ya tukio la Moto(Picha na Henry Chivihi)

Wananchi endeleeni kutumia namba 114 kutoa taarifa kwa wakati pindi tukio la moja linapotokea ili kusaidia jeshi la zimamoto na uokoaji kufika kwa wakati katika eneo la tukio

Na Musa Mtepa , Henry Abdala

Katika tukio la kusikitisha, nyumba moja inayomilikiwa na Bwana Msope, mkazi wa mtaa wa Ligula (Indian Kota) katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, imeungua kwa moto  Oktoba 31, 2024. Hadi sasa, chanzo cha moto hakijajulikana.

Kwa mujibu wa mke wa mwenye nyumba, Bi Jesca Msope, tukio hilo limetokea majira ya saa 9:45 jioni alipokuwa akimpatia chakula mjukuu wake.

Sauti ya 1 Bi Jesca Msope mke wa mwenye nyumba

Bi Jesca amesema aliona moshi na harufu ya kitu kinachoungua, hali iliyoleta taharuki.

Sauti ya 2 Bi Jesca Msope mke wa mwenye nyumba

Mamlo Mwenda, jirani wa nyumba hiyo, ameelezea kuwa walipogundua moshi, walikimbilia eneo la tukio na kuwasiliana na jeshi la zimamoto na uokoaji kwa msaada.

Sauti ya Mamlo Mwenda Jirani na mkazi wa mtaa wa Ligula (Indian Kota)

Kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mtwara, Mrakibu Msaidizi Oissa Singili, amethibitisha kupokea taarifa za tukio na kufika kwa wakati.

Sauti ya 1 Oissa Silingi mrakibu msadizi jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mtwara

 Aidha amesema kuwa wamefanikiwa kuuzima moto, na uchunguzi wa kutambua chanzo cha moto unaendelea.

Kaimu kamanda amewataka wananchi kuendelea kutumia namba ya dharura 114 ili kurahisisha shughuli za kuzima moto na maokozi.

Sauti ya 2 Oissa Silingi mrakibu msadizi jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mtwara

 Pia, amesisitiza umuhimu wa wananchi kukaa umbali wa mita 100 kutoka eneo la tukio na kushiriki kutoa taarifa kwa jeshi la zimamoto.

Sauti ya 3 Oissa Silingi mrakibu msadizi jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mtwara